• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kundi la IS nchini Libya linajipanga upya mwaka mmoja baada ya kupoteza ngome yake kuu nchini humo

  (GMT+08:00) 2017-12-07 16:49:55

  Wapiganaji wa kundi la IS waliobakia mjini Sirte, ambao ulikuwa ngome kuu ya kundi hilo nchini Libya, wanahamia kwenye maeneo ya misitu karibu na mji huo kwa lengo la kujipanga upya, ikiwa ni mwaka mmoja toka lipoteze ngome hiyo.

  Mwaka jana, vikosi vya Libya vinavyoungwa mkono na Umoja wa Mataifa vilitangaza kuudhibiti mji mzima wa Sirte baada ya mapigano yaliyodumu kwa miezi minane dhidi ya washirika wa kundi la IS ambapo askari zaidi ya 700 waliuawa na wengine 3,000 kujeruhiwa.

  Msemaji wa kikosi cha usalama cha Sirte Taha Hadid amesema, kiongozi wa ofisi ya uhamiaji ya kundi la IS Khabib Al-Darnawi, bado anaandikisha wanachama wapya, na kwamba anaongozana na wapiganaji wa kundi hilo waliobakia mjini Sirte na jangwa la Jufra.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako