• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Benki Kuu ya China yatetea utulivu wa mfumo wa kifedha baada ya tathmini ya IMF na Benki ya Dunia

  (GMT+08:00) 2017-12-07 16:50:31

  Benki Kuu ya China imesema inaamini utulivu wa mfumo wa kifedha wa nchi hiyo, ikiwa ni baada ya Shirika la Fedha la Kimataifa IMF na Benki ya Dunia WB kueleza hatari zinazoweza kutokea kwenye mfumo huo katika ripoti mbalimbali za tathmini.

  Benki hiyo imesema, ripoti hizo zimekubali kwa ujumla mafanikio ya China katika mageuzi ya hivi karibuni ya kiuchumi na kifedha, lakini kuna baadhi ya ufafanuzi na maoni kwenye ripoti hizo ambazo Benki hiyo haikubaliani nazo.

  Ripoti hizo ni sehemu ya Mradi wa Tathmini ya Sekta ya Fedha ya China, ambao ulizinduliwa mwaka 1990 na IMF pamoja na Benki ya Dunia ili kupima utulivu na uimara wa sekta ya fedha. Kwa mara ya kwanza, tathmini hiyo ilifanyika nchini China kuanzia mwaka 2009 – 2011.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako