• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Nigeria azindua mradi wa barabara iliyojengwa na kampuni ya China

  (GMT+08:00) 2017-12-07 18:06:32

  Rais Muhamadu Buhari wa Nigeria amekata utepe kuashiria kukamilika kwa mradi wa barabara iliyojengwa na Kampuni ya Uhandisi wa Ujenzi ya China CCECC mjini Kano, kaskazini mwa nchi hiyo.

  Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 2.1 inaunganisha barabara kuu mbili zinazoelekea nje ya mji huo, na mradi huu umekamilika kwa miezi minane kabla ya muda uliopangwa.

  Gavana wa jimbo la Kano Abdullahi Umar Ganduje ameishukuru kampuni ya China kwa kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha juu, na ubora wa ujenzi pia unasifiwa sana na wakazi wa huko.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako