• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China na Zimbabwe zasaini mikataba ya msaada

  (GMT+08:00) 2017-12-07 18:25:47
  Balozi wa China nchini Zimbabwe Bw. Huang Ping, na waziri wa fedha wa Zimbabwe Bw. Patrick Chinamasa, wametia saini mikataba mitatu ya ushirikiano kwa niaba ya serikali za nchi hizo mbili.. Mikataba iliyosainiwa ni pamoja na mkataba wa mfumo wa kutoa mikopo yenye unafuu kwa ajili ya ujenzi wa kuboresha uwanja wa ndege wa kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe, mkataba wa kusaidia Zimbabwe kujenga jengo jipya la bunge, na mkataba wa kusaidia ujenzi wa kipindi cha pili wa kituo cha kompyuta ya kiwango cha juu katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe. Katika hafla hiyo,Bw. Huang amesema China na Zimbabwe ni marafiki wa siku zote na katika siku zijazo, China itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya Zimbabwe na watu wake kutimiza ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kijamii. Kwa upande wake Bw. Chinamasa ameshukuru China kwa kutoa msaada kwa Zimbabwe. Pia amesema kuwa kama nchi kubwa ya pili kiuchumi duniani, China ina uzoefu wa maendeleo ya kiuchumi ambao unastahili kuigwa na Zimbabwe, na anatumai miradi zaidi ya ushirikiano inaweza kutekelezwa haraka iwezekanavyo.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako