• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampuni za China na Kenya zashirikiana kuzindua mtandao wa internet wa kasi zaidi na gharama nafuu

  (GMT+08:00) 2017-12-07 18:27:29

  Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Kenya ya Jamii imeingia ubia na kampuni ya China ya ZTE kutambulisha mtandao wa internet wa kasi zaidi na gharama nafuu hatua ambayo itasaidia kusambaza faida za matandao wa internet kwa watu wengi zaidi.

  Huduma za mtandao huo uliopewa jina la Faiba 4G, zitatolewa kwa kutumia namba za mwanzo za 0747, ambapo mteja anaweza kupiga simu bure, na baada ya uwekezaji wa dola za kimarekani milioni 50, mtandao huo utakuwa na uwezo kutoa sauti na picha za video zenye ubora wa juu.

  Kampuni ya Jamii imekuwa kampuni ya tano ya simu nchini Kenya, ikisaidia kuongeza ushindani kutokana na gharama za chini za simu za mkononi na huduma ya data nchini Kenya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako