• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nchi mbalimbali za Kiarabu zapinga Marekani kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel

  (GMT+08:00) 2017-12-07 19:06:36

  Umoja a Falme za Kiarabu (UAE) umezitaka nchi za Kiarabu na Kiislamu kuungana na kutangaza msimamo mmoja kutokana na hatua ya Marekani kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

  Rais Donald Trump wa Marekani ametangaza kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, na kuanza mpango wa kuhamisha ubalozi wa Marekani nchini humo uliopo Tel Aviv kwenda Jerusalem.

  Saudi Arabia imelaani uamuzi huo wa rais Trump kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, huku mahakama ya kifalme ya nchi hiyo ikionya kuwa uamuzi huo utakuwa na matokeo mabaya, ikiwa ni pamoja na kuongeza mvutano kati ya Palestina na Israel.

  Wizara ya mambo ya nje ya Kuwait imeeleza kuhuzunishwa na uamuzi huo wa Marekani, huku ikisema hatua hiyo ya upande mmoja imekiuka azimio lililotolewa na Umoja wa Mataifa kuhusu kuhakikisha hadhi ya kisiasa, kihistoria, kisheria na kibinadamu ya Jerusalem.

  Wizara ya mambo ya nje ya Iran imelaani vikali uamuzi wa rais Trump wa kuhamishia ubalozi wa Marekani nchin Israel kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem. Na Sudan pia imepinga uamuzi huo wa Marekani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako