• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mswada wa mifuko ya bure wapitishwa kwa wateja wa bidhaa

  (GMT+08:00) 2017-12-07 19:17:16

  Wawakilishi wa modi katika kaunti ya Uasin Gishu nchini Kenya wamepitisha mswada wa kuwaruhusu wateja wanaonunua bidhaa katika maduka ya jumla kupewa mifuko ya kubebea ya bure.

  Cahtherine Barmao aliyewasilisha mswada huo amesema wateja wamekuwa wakitozwa fedha nyingi sana kwa kuuziwa mifuko hiyo baada ya kununua bidhaa.

  Wawakilishi hao wamekubaliana kwamba kuna baadhi ya maduka ya jumla ,yanayotumia vibaya marufuku ya mifuko ya plastiki kwa kuuza mifuko mbadala kwa bei ghali.

  Wateja wamekuwa wakilalamikia bei hizo kote nchini Kenya wakidai imeaithiri bajeti zao .

  Mswada huu hata hivyo huenda ukafikishwa katika mabunge ya kaunti nyingine nchini Kenya kuwazuia wamiliki wa maduka ya jumla dhidi ya jambo hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako