• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wizara ya fedha kutia bilioni 77.4 kwa serikali za kaunti

  (GMT+08:00) 2017-12-07 19:17:41
  Hazina kuu ya serikali inatarajiwa kutoa shilingi bilioni 77.4 kwa serikali za kaunti nchini Kenya pindi Rais Uhuru Kenyatta atakapotia sahihi mswada wa marekebisho wa mapato ya kaunti.

  Baadfi ya fedha hizo ni miongoni mwa shilingi 345, zilizopendekezwa kutolewa kwa awamu kwa serikali za kaunti katika kutekeleza majukumu yake.

  Fedha hizi zilicheleweshwa awali kufuatia purukushani baina uongozi wa pande hizi mbili serikali kuu na zile za kaunti.

  Spika wa bunge la senate Ken Lusaka amesema wanatarajia Rais kuukubali mswada huo baada ya kuupitia kwa makini kwani utatoa mwelekeo wa jinsi raslimali zitakavyogawanywa.

  Mwenyekiti wa magavana nchini Kenya Josephat Nonok amesema miradi chungu mzima ya maendeleo yamekwama baada ya fedha hizo kucheleweshwa na serikali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako