• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri wa biashara aagiza bei ya sukari ipunguzwe.

  (GMT+08:00) 2017-12-07 19:18:12
  Waziri wa biashara nchini Uganda Amelia Kyambede amewataka watengenezaji sukari kupunguza bei ya bidhaa hiyo kwa wateja.

  Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari,waziri Amelia ameshtumu washikadau wa bidhaa hiyo kwa kuwaumiza wateja kwa bei ya juu ya sukari kwa zaidi ya miezi 8.

  Kilo moja ya sukari sasa inauzwa kwa shilingi 8500 kutoka 2500.

  Katika mkutano wa hivi karibuni baina bodi ya wauzaji sukari na wizara ya biashara ,wafanyibiashara hao wamekataa kuhusika kwenye bei hiyo.

  Wamejitetea kwamba bidhaa hiyo imeadimika na mahitaji yameongezeka ndio sababu ya ongezeko la bei.

  Wizara ya bishara ilipendekeza kuoagizwa sukari ya ziada kutoka nje jambo ambalo lilipingwa vikali na watengenezaji wa sukari wa ndani ya nchi hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako