• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mfumo wa kodi kurekebishwa

  (GMT+08:00) 2017-12-07 19:19:35

  Tanzania inapanga kupokea mapendekezo ya kuboresha mfumo wa kodi na usimamizi wake katika taifa ili kuchangia maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.

  Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango alisema hayo jana mjini hapa kwenye mkutano wa kujadili mchango wa sekta binafsi kwenye sera ya bajeti ya mwaka 2018/2019. Alisema serikali iko tayari kupokea mapendekezo kwenye kodi na usimamizi kwa lengo la kuboresha mfumo wa kodi katika nchi, uweze kutoa mchango unaotakiwa kuboresha maisha ya wananchi.

  Aidha katika mkutano huo alisihi wadau kupokea mapendekezo ya mfumo wa kodi ambao utaongeza nguvu kwa sekta binafsi.Msingi wa bajeti Akizungumza alisema kwamba kutokana na mazingira halisi yalivyo sasa, wadau wanastahili kuangalia kwa makini, mapendekezo na kuyajadili ili kuwa msingi wa bajeti ijayo kutokana na wahisani kupunguza mchango wao katika bajeti.

  Akizungumza mchango wa wahisani katika bajeti alisema kumekuwa na kushuka kwa misaada kutoka kwa washirika wa maendeleo kutoka Sh trilioni 1.5 mwaka 2013/2014 hadi kufikia Sh bilioni 495. Pia alisema hata mikopo ya masharti nafuu imeshuka kutoka Sh trilioni 1.258 mwaka 2013/2014 na kufikia Sh trilioni 1.231 mwaka 2015/2016.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako