• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Kagame ateuwa mawaziri wapy wa teknolojia na elimu

  (GMT+08:00) 2017-12-07 19:27:49

  Rais Paul Kagame wa Rwanda ameteuwa mawaziri wapya wawili wa elimu na mawasiliano.

  Eugine Mutimura ameteuliwa kuongoza wizara ya elimu akichukua nafasi ya Papias Musafiri nae Jean Dieu Rurangirwa akipewa wizara ya mawasailiano baada ya kupigwa kalamu Philber Nsengimana.

  Rwanda inalenga kuboresha sekta hizi mbili kwa lengo la kupata maendeleo ya uchumi.

  Mawaziri hawa wanatarajiwa kushirikiana kwa karibu na benki kuu ya dunia katika kutekeleza miradi tofauti ya maendeleo ya jamii.

  Wizara ya mawasiliano itaanza kutumia mfumo IFMIS katika utekelezaji miradi ya fedha,ushuru na bajeti kuu za serikali.

  Rwanda ni moja ya nchi zinazokua kwa kasi zaidi kiuchumi baranai Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako