• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kongamano la haki za binadamu la Kusini na Kusini lafanyika na kuhimiza maendeleo ya haki za binadamu ya nchi zinazoendelea

  (GMT+08:00) 2017-12-07 19:41:29

  Kongamano la haki za binadamu la Kusini na Kusini limefunguliwa leo hapa Beijing, likiwa na kauli mbiu ya "Kujenga Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja: Fursa Mpya kwa Maendeleo ya Haki za Binadamu ya Kusini na Kusini". Maofisa na wasomi wapatao mia tatu kutoka nchi na mashirika ya kimataifa zaidi ya 70 wamehudhuria kongamano hilo.

  Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya kupongeza kufunguliwa kwa kongamano hilo na kusisitiza kuwa maendeleo ya shughuli za haki za binadamu duniani hayatengani na juhudi za pamoja za nchi zinazoendelea, na kutarajia jamii ya kimataifa kufuata moyo wa usawa, haki, uwazi na ujumuishi, kuheshimu na kuonesha matarajio ya watu wa nchi zinazoendelea, kuhimiza watu wa nchi zinazoendelea wapate haki za binadamu katika sekta mbalimbali na kutimiza neema na maendeleo ya binadamu wote.

  Akitoa hotuba kwenye ufunguzi wa kongamano hilo, waziri wa mambo ya nje wa Surinam Bibi Yidiz Deborah Pollack-Beighle amesema kongamano la haki za binadamu la Kusini na Kusini limetoa fursa kwa maendeleo na ushirikiano kati ya nchi za Kusini, na nchi zinazoendelea zinaweza kutumia kongamano hilo kutoa maoni na kueleza ufuatiliaji wao juu ya mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya haki za binadamu, ili kuhimiza zaidi ushirikiano. Anasema,

  "Kongamano hilo linafanyika katika wakati mzuri, na limetupa fursa za kukutanisha nchi na wataalam wenye maoni yanayofanana. Naweza kusema tuko kwenye hatua muhimu ya kuingia kwenye enzi mpya ya shughuli za haki za binadamu. Naamini kuwa njia hiyo ya ushirikiano wa Kusini na Kusini inaweza kutuwezesha kupata njia mwafaka, na kuhakikisha kuwa tunaweza kuangalia na kushughulikia kwa haki masuala ya haki za binadamu bila upendeleo. Mbali na hayo, kongamano hilo pia limetoa jukwaa la majadiliano ya kiujenzi, hii ni muhimu kwa kila nchi na kila mwananchi kupata haki za kudumu za maendeleo."

  Naye mkurugenzi wa kituo cha haki za binadamu kati ya tamaduni tofauti katika Chuo Kikuu cha Uhuru cha Amsterdam Tom Zwart, amesema maendeleo ya haki za binadamu ya China sio tu yapo ndani ya nchi, bali pia yametoa mchango mkubwa kimataifa.

  "Katika miaka mitano iliyopita, China imefanya kazi kubwa na kujenga utaratibu wa kimataifa ulio na haki na masikilizano zaidi, na utaratibu huo unajumuisha utaratibu wa haki za binadamu wa kimataifa. Rais Xi Jinping wa China amesema suala la ukosefu wa uwakilishi na ujumuishi katika utaratibu wa usimamizi duniani linaweza kutatuliwa kupitia kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja. Naona kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja kunajumuisha sekta nyingi, ikiwa ni pamoja na sauti za watu wote kusikilizwa, na sio sauti za nchi zilizoendelea za Kaskazini tu. Tunahitaji busara na ujuzi wa nchi zote na jamii mbalimbali, haswa wa nchi za Kusini."

  Mtoa ripoti maalumu wa suala la haki za binadamu katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa Bw. Saad Alfaragi, amesema nchi za Kusini na Kusini zinaweza kufanya ushirikiano katika sekta mbalimbali, na pande mbalimbali zinatarajiwa kufikia maoni ya pamoja katika kongamano hilo.

  "katika sekta ya maendeleo, ushirikiano kati ya nchi za Kusini na Kusini ni mwingi, na umetoa njia za kupatikana kwa raslimali, na kuachana na njia ya jadi ya msaada wa maendeleo ambayo imeambatana na masharti mbalimbali. Ushirikiano kati ya Kusini na Kusini unaweza kusaidia nchi zinazoendelea kutimiza maendeleo ya binadamu kwa njia ya uvumbuzi, na kupata haki kamili za binadamu."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako