• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nigel Adkins awa kocha mpya wa Hull City

    (GMT+08:00) 2017-12-08 09:08:55

    Klabu ya Hull City ya Uingereza imemteua meneja wa zamani wa Southampton na Reading, Nigel Adkins kuwa mkufunzi wao mkuu kwa mkataba wa miezi 18.

    Adkins, mwenye miaka 52, anachukua nafasi ya Mrusi Leonid Slutsky aliyeiaga timu hiyo siku ya Jumapili, klabu hiyo ikiwa katika nafasi ya 20 katika ligi ya Championship. Adkins ambaye hakuwa kazini tangu kufutwa kwake na Sheffield United mwezi Mei 2016, aliwasaidia watakatifu hao wa St Marys kupanda ngazi hadi kwenye Ligi ya Premia mwaka 2012.

    Meneja huyo ataongoza mechi yake ya kwanza ugenini Brenford siku ya Jumamosi. Adkins alikuwa mlinda lango wa zamani wa Tranmere Rovers F.C. na Wigan na alihamia Southampton mwezi Septemba mwaka 2010.

    Baada ya kuwaongoza Southampton na kupanda ngazi ya kushiriki ligi ya Premia, alifutwa mwezi Januari mwaka 2013 huku Mauricio Pochettino akichukua nafasi yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako