• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zanzibar Heroes yailisha urojo Kilimanjaro Stars

    (GMT+08:00) 2017-12-08 09:09:13

    Timu ya taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) imekubali kipigo cha kwanza cha magoli 2-1 kwenye Mashindano ya kuwania ubingwa wa Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Senior Challenge Cup), dhidi ya 'Zanzibar Heroes'.

    Mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Kenyatta uliopo Machakos nchini Kenya, Kilimanjaro Stars ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la Wazanzibari kunako dakika ya 28 kupitia kwa Himid Mao kabla ya magoli mawili ya ushindi ya Zanzibar Heroes kufungwa kipindi cha pili.

    Matokeo mengine ya mechi za jana ni Burundi wameibuka na ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Ethiopia na mchezo kati ya Rwanda na Libya ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako