• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mavuno ya pamba Tanzania kuongezeka maradufu

    (GMT+08:00) 2017-12-08 20:00:18

    Tanzania inatarajia kuvuna tani 264,000 za pamba sawa na kilo milioni 264 katika msimu wa 2017/2018 kulinganisha na kilo milioni 70 za mwaka 2016/2017.

    Katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa kilichofanyika juzi katika ukumbi wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania,Ofisa Kilimo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ,Elias Kasuka ,alisema mkoa wa Simiyu una wakulima 301,000 watakaolima pamba katioka msimu huu kwa zaidi ya ekari 700,000 huku matarajio ya mavuno yakiwa zaidi ya kilo 700 kwa kila ekari moja.

    Alisema matarajio hayo yataufanya mkoa wa Simiyu kuwa na mavuno mengi na kujipatia kipato kikubwa kitokanacho na pamba tofauti na msimu uliopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako