• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baiskeli: Rwanda timu pekee Afrika Mashariki itakayoshiriki masindano ya kimataifa Gabon

    (GMT+08:00) 2017-12-11 10:14:17

    Rwanda ni taifa pekee kutoka Afrika Mashariki lililoorodheswa katika timu za mataifa yatakayoshiriki mashindano ya kimataifa ya mbio za baiskeli yatakayofanyika januari mwaka 2018 nchini Gabon.

    Katika mbio hizo zitakazoshirikisha timu 16, timu ya Rwanda inatarajiwa kuongozwa na nyota sita akiwemo Bonaventure Uwizeyimana ambaye katika mbio kama hizi msimu uliopita alishinda nafasi ya sita.

    Timu zingine zinazoshiriki michuano hiyo ni wenyeji Gabon, Burkina Faso, Cameroon, Ivory Coast, Eritrea, Ethiopia, Morocco, Mauritius, Rwanda, Tunisia, Ufaransa, Italy, Ureno na Ujerumani.

    Mbio hizo maarufu kama (Tropicale Amissa Bongo) zinatarajiwa kufanyika rasmi Januari 15 hadi 21 mwaka 2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako