• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Cecafa: Kenya kuamua hatma yake ya kufuzu kwenye mechi dhidi ya Libya

    (GMT+08:00) 2017-12-11 10:14:56

    Ili kufuzu hatua ya nusu fainali, Harambee Stars watalazimika kupata ushindi kwenye mechi yao ya mwisho ya hatua ya makundi ya michuano ya kombe la CECAFA watakapocheza leo dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania ambayo haina nafasi ya kufuzu.

    Kenya wako nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi A la michuano hiyo wakiwa na pointi 5, ambazo bado zinaweza kufikiwa na Libya yenye pointi 3, ambayo inashuka dimbani leo kucheza na vinara wa kundi hilo Zanzibar Heroes ambao tayari wamefuzu

    Nako kwenye kundi B, la michuano hiyo, kuna Mechi moja ya kukamilisha mzunguko inachezwa mjini Kakamega baina ya Burundi na Sudan Kusini, Burundi wana alama 4 sawa na Ethiopia lakini wakiwa juu kwenye msimamo kufuatia tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, lakini Uganda ndiyo timu pekee iliyofuzu kwenye nusu fainali kutoka kundi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako