• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China na Afrika kuhimiza ushirikiano wa kilimo

  (GMT+08:00) 2017-12-11 18:27:51

  Kongamano la 4 la ushirikiano wa kilimo kati ya China na Afrika limefanyika leo mjini Haikou, mkoani Hainan, China.

  Mwanachama wa kikundi cha uongozaji cha chama cha kikomunisti cha China katika wizara ya kilimo ya China Bw. Bi Meijia amesema, katika miaka ya hivi karibuni, chini ya mfumo ya "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, wizara ya kilimo ya China imeharakisha mchakato wa ushirikiano wa kilimo kati ya pande hizo mbili. Pia wizara hiyo imeimarisha msingi wa uungaji mkono kutoka watu wa pande hizo mbili, na kufanya msaada wa ufundi, ujenzi wa uwezo, uwekezaji wa kilimo na ushirikiano wa kusini na kusini kupata ufanisi na maendeleo na kupanuka zaidi.

  Amesema, sekta ya kilimo ni sekta inayohusiana na maisha ya watu, inafuatiliwa na China na Afrika, na kwamba kuzidisha ushirikiano wa kilimo ni muhimu kwa kuinua uwezo wa kujiendeleza wa kilimo wa nchi za Afrika na kujenga mustakabali wa pamoja wa China na Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako