• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Biashara kati ya China na nchi za nje zaongezeka kwa haraka

  (GMT+08:00) 2017-12-12 17:52:32

  Katika miezi 11 iliyopita ya mwaka huu, thamani ya biashara kati ya China na nchi za nje imeongezeka kwa haraka, huku muundo wa biashara ukiendelea kuboreshwa, na mwelekeo mzuri umeimarishwa zaidi. Ofisa mwandamizi husika wa idara ya biashara za nje ya wizara ya biashara ya China ameeleza kuwa, hali hii inatokana na sababu mbalimbali zikiwemo ubora wa sera, ukuaji wa uchumi, na marekebisho ya muundo wa mashirika. Anakadiria kuwa mwakani biashara kati ya China na nchi za nje zitadumisha hali nzuri.

  Takwimu zilizotolewa na forodha zinaonesha kuwa, kuanzia mwezi Januari hadi Novemba, thamani ya biashara kati ya China na nchi za nje ilifikia renminbi yuan trilioni 25.14, sawa na dola za kimarekani trilioni 3.8, ambalo ni ongezeko la asilimia 15.6 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu. Miongoni mwa biashara hizo, thamani ya bidhaa zilizouzwa na China katika nchi za nje ni yuan trilioni 13.85, na kuongezeka kwa asilimia 11.6, huku thamani ya bidhaa zilizoagizwa kutoka nchi za nje ni yuan trilioni 11.29, na kuongezeka kwa 20.9. Urari mzuri ni yuan trilioni 2.56, na kupungua kwa asilimia 16.7 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu.

  Mshauri mwandamizi wa idara ya biashara za nje ya wizara ya biashara ya China Bw. Song Xianmao amechambua akieleza kuwa, ongezeko la kasi la biashara kati ya China na nchi za nje katika miezi 11 iliyopita ya mwaka huu, hasa linatokana na hali nzuri ya soko la kimataifa, pamoja na ukuaji mzuri wa uchumi wa China. Anasema,

  "Thamani ya uzalishaji mali nchini China imeendelea kudumisha ongezeko la kasi kubwa ya kati. Kuanzia mwezi Januari hadi Oktoba, uwekezaji kwenye mali zisizohamishika uliongezeka kwa asilimia 7.3, na kielezo cha wasimamizi wa manunuzi PMI cha mwezi Novemba ni 51.8. Hali nzuri ya ukuaji wa uchumi wa China imesababisha ongezeko la manunuzi kutoka nchi za nje. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Shirika la Biashara la kimataifa WTO, kasi ya ongezeko la manunuzi ya China kutoka nchi za nje inazidi kidhahiri wastani wa dunia nzima, hata kuliko Marekani, Ujerumani, Japan ambazo ni nchi zinazodumisha thamani kubwa ya biashara na nchi za nje."

  Mwaka huu, wizara ya biashara, idara nyingine husika za serikali kuu pamoja na maeneo mbalimbali nchini China zimetekeleza kwa makini sera zilizotolewa na baraza la serikali katika kuhimiza biashara za nje, kwa hatua za kupunguza mizigo ya makampuni, na kuboresha mazingira ya biashara, ili kudhihirisha zaidi ufanisi wa sera hizo.

  Bw. Song anaona kuwa mbali na sera nzuri, makampuni ya China yamerekebisha muundo, hali ambayo pia ni sababu ya kuhimiza ongezeko la biashara za nje. Anasema,

  "kutokana na maendeleo ya shughuli mpya na uboreshaji wa mfululizo wa mazingira ya biashara za nje, kasi za ongezeko la biashara za kuvuka mipaka kupitia tovuti za Internet na manunuzi katika soko za nje zimezidi kasi ya ongezeko la jumla. Hali ambayo ni mvuto mpya wa ongezeko la biashara za nje. Makampuni mengi ya China yameongeza uwezo wao wa ushindani katika soko la kimataifa kwa kufanya uvumbuzi na marekebisho ya muundo wa matoleo."

  Takwimu zinaonesha kuwa kuanzia mwezi Januari hadi Novemba mwaka huu, thamani ya mauzo ya makampuni binafsi katika nchi za nje ilifikia yuan trilioni 6.46, ambalo ni ongezeko la asilimia 13.8 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu. Bw. Song anaona hali ya biashara kati ya China na nchi za nje inatarajiwa kudumisha mwelekeo mzuri. Anasema,

  "Katika miaka kadhaa iliyopita, makampuni yetu yamefanya kazi nyingi katika kurekebisha muundo wa matoleo na injini ya kujiendeleza ili kukabiliana na mabadiliko ya soko la kimataifa. Naamini kuwa hali ya biashara kati ya China na nchi za nje itaendelea kuwa nzuri."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako