• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Kenya aahidi kuweka mkazo katika umoja wa taifa na ukuaji wa uchumi

    (GMT+08:00) 2017-12-13 09:54:53

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameahidi kuweka mkazo katika ukuaji wa uchumi, na kushirikiana na wakenya wote katika muhula wake wa pili na wa mwisho madarakani.

    Rais Kenyatta amesema hayo kwenye sherehe ya maadhimisho ya 54 ya Siku ya Uhuru ya Kenya mjini Nairobi, akitangaza vipaumbele vinne vya kuhimiza ukuaji wa uchumi, kuwa ni usalama wa chakula, nyumba za bei nafuu, viwanda, na utoaji wa huduma nafuu za afya.

    Rais Kenyatta amesema kazi hizo muhimu zitatoa nafasi za ajira zitakazokidhi mahitaji ya kimsingi ya wananchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako