• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Mauritius zaanzisha rasmi mazungumzo kuhusu mkataba wa biashara huria

    (GMT+08:00) 2017-12-13 09:55:22

    Wakati wa Mkutano wa 11 wa mawaziri wa Shirika la biashara duniani WTO, naibu waziri wa biashara wa China Bw. Wang Shouwen na balozi wa Mauritius katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Bw. Israhyananda Dhalladoo, wamesaini makubaliano kuhusu Mkataba wa biashara huria kati ya China na Mauritius iliyopitishwa na Wizara ya biashara ya China na Wizara ya mambo ya nje, ushirikiano wa kikanda na biashara ya kimataifa ya Mauritius, na kutangaza rasmi kuanzishwa kwa mazungumzo kuhusu mkataba wa biashara huria kati ya pande hizo mbili.

    Hili litakuwa eneo la kwanza la biashara huria kati ya China na nchi ya Afrika. Baada ya kuanzishwa kwake, si kama tu litapanua mawasiliano na uwekezaji kati ya pande hizo mbili, bali pia litatoa msukumo mpya katika kuhimiza uhusiano kati ya China na Afrika, na kusukuma mbele utekelezaji wa pendekezo la "Ukanda mmoja, Njia moja" barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako