• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yachukua nafasi muhimu katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu ya UM

    (GMT+08:00) 2017-12-13 10:01:42

    Mwenyekiti wa Kikao cha 72 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Bw. Miroslav Lajcak, amesema China imechukua nafasi muhimu katika kuhimiza utekelezaji wa malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu hadi mwaka 2030.

    Bw. Lajcak amesema China si kama tu imejiendeleza kiuchumi, bali pia inafanya juhudi kuzisaidia nchi nyingine, na kugharimia dola bilioni 3 za kimarekani katika kuanzisha Mfuko wa ushirikiano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa kati ya nchi za Kusini-Kusini, hatua ambayo imefurahiwa na jumuiya ya kimataifa.

    Amesema anatumaini kuwa China ikiwa moja kati ya nchi tano wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, itatoa mchango mkubwa zaidi katika mambo ya Umoja wa Mataifa na dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako