• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Masumbwi Kimataifa, Bondia Tyson Fury asema atakapofunguliwa ataanza na Anthony Joshua

    (GMT+08:00) 2017-12-13 10:37:48

    Baada kupunguziwa adhabu ya kupatikana na dawa zisizoruhusiwa michezoni, bondia Tyson Fury ameweka wazi nia ya kutaka kupigana na mwingereza mwenzake Anthony Joshua kwa kile alichodai kuwa anataka kurejesha ubingwa wake wa mikanda ya IBF and WBA katika uzito wa juu.

    Mwaka 2016, Fury alinyang'anywa leseni ya ubondia pamoja na kuvuliwa mikanda yote aliyokuwa ameshinda ikiwemo ya ubingwa wa uzito wa juu baada ya kuingia mgogoro na bodi inayosimamia mchezo wa masumbwi nchini Uingereza baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa zisizoruhusiwa michezoni.

    Sasa baada ya jana kutangaziwa kuwa adhabu yake imepunguzwa hadi kipindi cha miaka miwili, tayari Fury ameanza mikakati na tambo za kurejea ulingoni na akidai amepania kurejesha ubingwa wake, na mara ya mwisho kupanda ulingoni ikiwa ni Novemba 2015 alipomshinda Vladimir Klitschko wa Ukraine mjini Dusseldorf nchini Ujerumani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako