• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hafla ya kukumbuka mauaji ya Nanjing yafanyika mjini Nanjing, China

    (GMT+08:00) 2017-12-13 17:38:57

    Huu ni mwaka wa 80 tangu kutokea kwa mauaji ya Nanjing. Hafla kubwa ya kukumbuka mauaji hayo imefanyika leo asubuhi mjini Nanjing, China, na kuhudhuriwa na watu wengi akiwemo rais Xi Jinping.

    Hafla ya kukumbuka mauaji ya Nanjing imefanyika katika jumba la makumbusho la wachina waliouawa na wavamizi wa Japani katika mauaji ya Nanjing. Katika uwanja wa jumba hilo, bendera imepepea nusu mlingoti, huku wajumbe elfu 10 kutoka hali mbalimbali wakiwemo maofisa waandamizi wa serikali kuu ya China walioongozwa na rais Xi Jinping wakisimama kimya.

    Wanajeshi 18 kutoka majeshi ya majini, nchi kavu na anga ya China wamefanya gwaride. Tarehe 13, Desemba miaka 80 iliyopita, wavamizi wa Japan waliingia Nanjing ambao ulikuwa mji mkuu wa China wakati huo, na kuwaua wachina laki tatu wakiwemo wanajeshi wa China waliokamatwa pamoja na raia wa kawaida. Mauaji hayo ambayo ni kinyume na ubinadamu ni maumivu ya daima ya taifa la China. Mwezi Februari mwaka 2014, China ilitunga sheria ya kuiweka tarehe 13, Desemba kuwa ni siku ya kitaifa ya kukumbuka watu waliouawa katika mauaji ya Nanjing.

    Hafla ya kukumbuka mauaji hayo ya mwaka huu imeanza saa nne kamili. Watu waliohudhuria hafla hiyo waliimba wimbo wa taifa kwa pamoja, halafu walitoa rambirambi kwa kusimama kimya, huku king'ora cha kutahadharisha mashambulizi ya anga kikilia.

    Wakati huo huo, milio hiyo pia ilisikika kote mjini Nanjing, pamoja na milio ya honi za magari, magarimoshi na meli. Watu waliokuwa wakitembea walisimama, ili kuwakumbuka watu waliouawa katika mauaji ya Nanjing, pamoja na wengine wengi zaidi waliouawa na wavamizi wakati wa vita kuu ya pili.

    Kwa kufuata muziki wa maombolezo, wanajeshi 16 wakibeba mashada manane makubwa ya maua walikwenda juu ya jukwaa, na kuyaweka mashada hayo mbele ya "Ukuta wa Maafa" wenye majina ya baadhi ya watu waliouawa. Kisha vijana na watoto 80 wa Nanjing, walisoma Azimio la Amani kwa pamoja.

    Mwenyekiti wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bw. Yu Zhengsheng kwenye hotuba yake amesema, kufahamu vizuri historia ni sharti la lazima katika kuanzisha mustakabali mzuri zaidi. Tunapaswa kukumbuka historia na hadithi za mababu zetu kwa ajili ya mustakabali wetu mzuri na watoto wetu. Tutajitahidi kutimiza amani ya muda mrefu na hata ya daima kwa ajili ya binadamu wote bila kuchoka, ili kuepuka kutokea tena kwa maafa ya kihistoria. Ili kutimiza lengo hilo, China itashikilia njia kujipatia maendeleo kwa amani, na haitakuwa nchi ya kimwamba na kutovamia nchi nyingine daima, kwani haitaki nchi nyingine zikabiliwe na maafa yaliyoikumba.

    Shughuli hiyo ilimalizika kwa wajumbe 6 kugonga kengele kubwa ya amani, huku njiwa 3,000 wakiruka kwa pamoja, kumaanisha kumbukumbu kwa watu laki tatu waliouawa, na nia imara ya wananchi wa China ya kustawisha taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako