• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Liu Yandong ahimiza kuchangia ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja

    (GMT+08:00) 2017-12-13 17:47:55

    Mkutano wa 12 wa chuo kikuu cha Confucius duniani tarehe 12 ulifanyika huko Xi'an na kuhudhuriwa na wakuu wa vyuo vikuu na wajumbe wa vyuo vya Confucius kutoka nchi na sehemu zaidi 140.

    Akizungumza kwenye mkutano, Naibu waziri mkuu wa China ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya makao makuu ya chuo kikuu cha Confucius Bibi Liu Yandong amesisitiza kuwa, chuo hicho kinapaswa kufanya juhudi ili kuongeza urafiki na ushirikiano wa kunufaishana kwa kupitia mawasiliano ya lugha na kujifunza utamaduni kutoka kila upande, na kutoa mchango kwa kuunda jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu.

    Wajumbe wa mkutano huo wamesifu mawazo ya rais Xi Jinping wa China kuhusu pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja, na wameahidi kufanya juhudi kujiunga na shughuli hiyo na kuimarisha ushirikiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako