• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ubalozi wa Marekani nchini Israel hautaweza kuhamia Jerusalem kabla ya mwaka 2020

    (GMT+08:00) 2017-12-13 17:56:31

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson amesema, ubalozi wa nchi hiyo nchini Israel hautahamia mjini Jerusalem kabla ya mwaka 2020.

    Gazeti la New York Times la Marekani limemnukuu waziri huyo akisema, uhamisho huo sio kitu kitakachotokea mara moja, na kwamba hauwezi kufanyika kabla ya miaka mitatu au zaidi.

    Jumatano iliyopita rais Donald Trump wa Marekani alitangaza kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel na nia yake ya kuhamisha ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem.

    Wakati huohuo, viongozi na maofisa wa ngazi ya juu kutoka nchi za Kiislam wanatarajiwa kufanya mkutano wa dharura hii lo mjini Istanbul, Uturuki kujadili uamuzi wa Marekani wa kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako