• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China inapenda kushirikiana na Russia na pande nyingine kusukuma mbele mchakato wa kisiasa wa suala ya Syria

    (GMT+08:00) 2017-12-13 18:20:49

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang leo hapa Beijing amesema, China inapenda kushirikiana na Russia na pande nyingine kufanya juhudi kwa ajili ya kusukuma mbele mchakato wa kutatua suala la Syria kwa njia ya kisiasa.

    Bw. Lu Kang amesema, katika miaka ya hivi karibuni mapambano dhidi ya ugaidi nchini Syria yamepata maendeleo muhimu. Amesema China inaitaka jumuiya ya kimataifa kuendelea kusawazisha ushirikiano, kupinga ugaidi wa aina yoyote, na kusukuma mbele mchakato wa kutatua suala la Syria kwa njia ya kisiasa chini ya uongozi wa Umoja wa Mataifa.

    Hivi karibuni, Rais Vladimir Putin wa Russia alitangaza kuondoa jeshi la nchi yake kutoka Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako