• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afreximbank yatoa dola bilioni 1.5 kwa Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2017-12-13 19:27:23

    Benki ya Uagizaji na Uingizaji barani Afrika (Afreximbank) itatoa mkopo wa dola za kimarekani bilioni 1.5 kuunga mkono juhudi za kufufua uchumi wa Zimbabwe.

    Gazeti la nchini humo The Herald limesema, fedha hizo zitatumika kufufua sekta ya uzalishaji na kuchochea uagizaji zaidi.

    Rais wa Benki hiyo Okey Oramah amesema, Benki yake ina shauku ya kusaidia uchumi wa Zimbabwe kwa kutoa fedha zaidi ili kupunguza msongamano katika benki, na pia kuunga mkono akaunti za fedha za kigeni katika benki ili kuhakikisha wale wanatumia dola ya kimarekani wanaweza kuzitumia katika kulipia bidhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako