• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Polisi watano wauawa katika shambulizi la kujitoa mhanga nchini Somalia

  (GMT+08:00) 2017-12-14 18:13:02

  Askari polisi watano wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulizi la kujitoa mhanga lililotokea katika chuo cha polisi mjini Mogadishu nchini Somalia.

  Askari polisi mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema, mlipuaji huyo aliyevalia sare za polisi alilipua mabomu aliyovaa wakati wa gwaride la asubuhi kwenye chuo cha polisi cha General Kayire kilichoko Mogadishu. Amesema shambulizi hilo limetokea wakati polisi wakifanya mazoezi kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Polisi iliyopangwa kufanyika tarehe 20 mwezi huu.

  Hakuna kundi lililokiri kuhusika na shambulizi hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako