• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka Cecafa, Kenya wafuzu fainali baada ya kuifunga Burundi

    (GMT+08:00) 2017-12-15 10:26:20

    Timu ya taifa ya Kenya imefanikiwa kufuzu fainali ya michuano ya CECAFA baada ya kushinda mechi ya nusu fainali kwa goli moja kwa sifuri ilipocheza na Burundi mjini Kisumu.

    Goli hilo la ushindi la Harambee stars lilipatikana kunako dakika ya 97 kupitia mchezaji wa klabu ya AFC Leopards Whyvonne Isuza.

    Licha ya kuwapongeza vijana wake kufuatia ushindi huo, kocha mkuu wa Stars, Paul Put, amekiri kuwa Burundi pia wamefanikiwa kufikia viwango vya juu vya soka.

    Naye Kocha wa Burundi, Niyungeko Olivier, amewasihi wachezaji wake kutovunjika moyo na kuwataka waufikirie mchezo wa ujao wa kusaka mshindi wa tatu.

    Kenya wanasubiri kucheza mechi ya fainali dhidi ya mshindi katika mechi ya nusu fainali inayopigwa leo kati ya Uganda na timu ya taifa ya Zanzibar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako