• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo ya tisa ya uchumi na mambo ya fedha kati ya China na Uingereza yafanyika Beijing

    (GMT+08:00) 2017-12-16 19:21:46

    Naibu waziri mkuu wa China Bw. Ma Kai na waziri wa fedha wa Uingereza Bw. Philip Hammond wameongoza kwa pamoja mazungumzo ya tisa ya uchumi na mambo ya fedha kati ya China na Uingereza leo hapa Beijing.

    Bw. Ma amesema huu ni mwaka wa 45 baada ya China na Uingereza kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia kwenye ngazi ya ubalozi, na kuimarisha ushirikiano wa kivitendo kati ya pande hizo kuna fursa mpya. Amesema mazungumzo hayo ni ya kwanza ya uchumi na mambo ya fedha kufanyika kati ya nchi hizo mbili baada ya mkutano mkuu wa 19 wa chama cha Kikomunisti cha China kumalizika hivi karibuni, na yanabeba majukumu ya kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili na kupanua ushirikiano wa uchumi na mambo ya fedha kati ya China na Uingereza katika kipindi kipya cha historia. Ameongeza kuwa China inapenda kushirikiana na Uingereza kuingiza mambo mapya kwa "zama za dhahabu" katika uhusiano wa China na Uingereza na kuinua uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati yao kwenye kiwango kipya.

    Kwa upande wake, Bw. Hammond amesema Uingereza inaunga mkono pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kutarajia kushirikiana na China kutumia vizuri fursa zilizopo na kuimarisha ushirikiano wa kivitendo katika Nyanja mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako