• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Kenya washinda ubingwa wa mshindano ya Cecafa 2017

    (GMT+08:00) 2017-12-18 10:31:40

    Timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars ndio mabingwa wa michuano ya 39 ya mpira wa miguu kwa mataifa ya Afrika Mashariki na kati iliyomalizika jana mjini Nairobi, kufuatia ushindi iliopata dhidi Zanzibar kwenye mechi ya fainali.

    Hii ni mara ya saba kwa Kenya kuwahi kutwaa ubingwa huo tangu waanze kushiriki mashindano hayo mwaka 1926.

    Kutokana na ushindi wa jana, Kenya wamezawadiwa kombe, medali pamoja na dola za kiMarekani 30,000, wakati washindi wa pili Zanzibar Heroes wakipatiwa medali na dola 20,000 huku washindi wa tatu Uganda wakipewa medali na dola 10,000.

    Mchezaji bora wa mashindano ni Golikipa wa Harambee Stars, Patrick Matasi, na mchezaji wa Derrick Nsibambi alishinda kiatu cha dhahabu kutokana na kuwa mfungaji wa magoli mengi kwenye mashindano.

    Katika mechi ya fainali iliyofanyika kwenye uwanja wa machakos, Kenya iliwabidi kusubiri mikwaju ya penati baada ya matokeo muda wa dakika tisini za kawaida na muda wa nyongeza kuwa sare ya magoli 2-2.

    Shujaa katika mikwaju ya penati alikuwa golikipa wa Harambee Stars ambaye alifanikiwa kuokoa tatu zilizopigwa na Heroes, zikiwemo za Adeyum Sief, Issa Dau na Issa Juma.

    Lakini licha ya kupoteza kwenye mchezo wa fainali, kocha mkuu wa Zanzibar Heroes Hemed Suleiman Ali 'Morocco' amewapongeza vijana wake, huku akisema kuwa, anajivunia mafanikio aliyoyapata ikiwa ni kuifikisha fainali timu yake ingawa hakufanikiwa kutwa taji hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako