• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China itaendelea kuunga mkono huduma za kifedha kwa makampuni

    (GMT+08:00) 2017-12-18 16:28:26

    Mkutano wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC uliomalizika hivi karibuni umepanga mpango wa jumla wa kazi za uchumi kwa mwaka 2018, na kuweka wazi kuwa, ili kuzuia kutokea kwa hatari kubwa za kifedha mwakani, ni lazima kuunga mkono huduma za kifedha kwa makampuni.

    Kuhusu ni makampuni gani yatakayopata huduma zaidi za kifedha, mwenyekiti wa Tume ya Usimamizi wa Mambo ya Benki ya China Bw. Guo Shuqing anasema, "China inatakiwa kufanya vizuri kazi za kiuchumi za kuyahudumia makampuni, kuunga mkono benki kuzisaidia taasisi za kifedha zinazonufaisha watu wengi, kuunga mkono ukusanyaji fedha kwa makampuni madogo, sekta ya kilimo, na kuondoa umaskini. Pia kuendelea kuunga mkono miradi ya ustawi wa jamii ukiwemo ujenzi wa miundombinu na miradi ya makazi."

    Hivi sasa, baadhi ya makampuni ya China yanakabiliwa na hatari ya madeni. Mtafiti wa mambo ya fedha katika Chuo Kikuu cha Renmin cha China Dong Ximiao amesema tatizo hilo linahusika na jinsi makampuni ya China yanavyokusanya fedha. Anasema, "Ni lazima kuondoa matumizi mabaya ya njia za kifedha na kuondoa uwezo wa kupita kiasi wa uzalishaji. Makampuni ambayo shughuli zake zimekuwa au zinakaribia kusimama yanapaswa kufungwa badala ya kutegemea msaada wa serikali. Pia tunaweza kuyageuzi madeni ya makampuni yanayofanya vizuri kuwa hisa."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako