• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China imesajili zaidi ya watu milioni 67 wa kujitolea

    (GMT+08:00) 2017-12-18 17:51:49

    Shirikisho la Huduma za Kujitolea la China limesema, idadi ya watu wa kujitolea waliosajiliwa nchini humo imepita milioni 67.

    Akizungumza kwenye mkutano wa bodi ya wakurugenzi ya Shirikisho hilo waliokutana leo hapa Beijing, makamu mkuu wa Shirikisho hilo Zhao Jinfang amesema, asilimia 49 ya watu wanaojitolea wana umri wa chini ya miaka 35. Amesema idadi ya mashirika yanayotoa huduma za kujitolea yamepita laki nne, huku zaidi ya miradi milioni 1.03 ya kujitolea imeanzishwa.

    Zhao amesema, takwimu hizo zinatokana na mfumo wa taarifa kwa huduma za kujitolea nchini China uliozinduliwa hivi karibuni, ambao umekubaliwa na wizara ya masuala ya kijamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako