• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Bidhaa za Rwanda zaonyeshwa kwenye maonyesho ya Misri

    (GMT+08:00) 2017-12-18 19:12:25

    Bidhaa za Rwanda kwa mara ya kwana zimeonyeshwa kwenye maonyesho ya Misri katika hatua ya kupanua upatikanaji wa soko kwa bidhaa hizo.

    Maonyesho hayo yanayofanyika Rwanda yanahudhuriwa na waonyeshaji kutoka misri na eneo la mashariki ya kati.

    Mratibu wa maonyesho hayo Natacha Haguma, amesema yanatoa fursa ya kipekee kwani kwa mara ya kwanza bidhaa zinazotengenezwa nchini Rwanda zimepewa nafasi.

    Amesema yatatoa fursa kwa watengenezaji wa Rwanda pamoja na wenye biashara kukutana na washirika wapya.

    Maonyesho hayo ni ya siku 16 na yalianza Desemba 15 katika jumba la Petit Stade mjini Kigali.

    Sasa kuna jumla ya waonyeshaji bidhaa wapatao 56 ikilinganishwa na 46 ya mwaka jana.

    Waonyeshaji wengine ni kutoka Iran, Pakistan, Syria, India, Dubai na Singapore.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako