• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 6 wafariki na wengine 22 kujeruhiwa baada ya treni kuacha njia nchini Marekani

    (GMT+08:00) 2017-12-19 08:52:05

    Watu wasiopungua sita wamefariki dunia na wengine 22 wamekimbizwa katika hospitali tatu baada ya treni moja ya Amtrak kuacha njia kusini mwa Seattle, jimboni Washington, Marekani. Kikosi cha Doria cha Jimbo la Washington kimesema mabehewa 13 kati ya 14 ya treni nambari 501 ya Amtrak, yaliacha njia na behewa moja liliaguka katika barabara kuu yenye magari mengi, na magari matano na nyumba mbili ziliharibiwa. Bodi ya Usalama wa Usafiri ya Marekani imesema bado ni mapema kusema kama ajali hiyo imesababishwa na mwendo wa kasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako