• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapalestina wasema kura ya turufu ya Marekani kwenye azimio kuhusu Jerusalem itasababisha kutengwa zaidi

    (GMT+08:00) 2017-12-19 09:21:56

    Mamlaka ya Palestina imeilaumu Marekani kwa kulipigia kura ya turufu azimio la baraza la usalama kuhusu mji wa Jerusalem, na kusema hatua hiyo itafanya Marekani itengwe zaidi na jumuiya ya kimataifa.

    Jana Marekani iliipigia kura ya turufu rasimu ya azimio lililopendekezwa na Misri, linalopinga Marekani kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel. Msemaji wa rais wa Palestina Bw Abu Rudeineh, amesema hatua ya Marekani imeenda kinyume na makubaliano ya kimataifa, na inaunga mkono ukaliaji na uvamizi.

    Rais Mahmud Abbas wa Palestina alitangaza kuwa wapalestina wataomba uanachama kamili kwenye Umoja wa Mataifa ili kujibu hatua ya Marekani kuhusu Jerusalem.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako