• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wahimiza ushirikiano wa kimataifa ili kufanya uhamiaji dunia kuwa salama.

    (GMT+08:00) 2017-12-19 09:22:16

    Umoja wa Mataifa umetoa mwito wa kuwepo kwa ushirikiano ili kusimamia uhamiaji ambao manufaa yake yanaenezwa kwa upana, na haki za binadamu za wahamiaji zinalindwa.

    Akiongea jana tarehe 18 kwenye maadhimisho ya Siku ya Wahamiaji Duniani, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema kuwa Umoja huo unatambua mchango wa wahamiaji milioni 258, na ushahidi unaonyesha kuwa wahamiaji wanatoa mchango kiuchumi, kijamii na kiutamaduni kwenye jamii wanazoishi

    Amesema uhamiaji ulikuwepo tangu zamani, na kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, idadi ya watu, kukosekana kwa utulivu na mahitaji ya nguvu kazi, uhamiaji utaendelea kuwepo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako