• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jamii ya kimataifa yatoa wito wa kumaliza suala la Jerusalem kwa njia ya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2017-12-19 17:47:44

    Jamii ya kimataifa imetoa wito kwa pande zinazohusika kufanya majadiliano ili kuamua hadhi ya Jerusalem baada ya Marekani kupiga kura ya veto dhidi ya muswada wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo jana.

    Balozi wa Misri kwenye Umoja wa Mataifa, Amr Abdelatif Aboulatta amesema, muswada wa azimio hilo unalenga kuhakikisha kuwa juhudi zozote za kubadili hadhi au jamii ya Mji wa Kale wa Jerusalem hazitakuwa na athari yoyote, hazitambuliki, na lazima zikemewe. Nchi nyingine 14 wajumbe wa Baraza la Usalama walipiga kura kukubali waraka huo ulioandikwa na Misri lakini kwa kuwa Marekani ni mjumbe wa kudumu wa Baraza hilo ina nguvu ya kura ya veto, muswada wa azimio hilo ulishindwa kupitishwa.

    Kaimu balozi wa China kwenye Umoja wa Mataifa Wu Haitao amesema, muswada wa azimio uliowasilishwa jana kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaendana na maazimio mengine ya Baraza hilo na ni mwendelezo wa maudhui na nia ya maazimio yaliyopita. Amesema siku zote China inaunga mkono na kusukuma mbele mchakato wa mazungumzo ya amani ya Mashariki ya Kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako