• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Dunia yapandisha makadirio yake kuhusu ukuaji wa uchumi wa China kwa mwaka huu hadi asilimia 6.8

    (GMT+08:00) 2017-12-19 18:19:50

    Benki ya Dunia (WB) imetoa ripoti fupi kuhusu uchumi ya China, ikikadiria kuwa uchumi wa China utaongezeka kwa asilimia 6.8 mwaka huu, 0.1% juu zaidi ikilinganishwa na makadirio yaliyotolewa mwezi Oktoba.

    Ripoti inaonyesha kuwa, kutokana na kufufuka kwa biashara ya kimataifa, uuzaji wa bidhaa kwa nje umechangia ukuaji wa uchumi wa China kwa robo tatu mfululizo, hivyo kuongeza imani ya makampuni, na fursa za ajira zimeendelea kuongezeka, huku mwelekeo wa mitaji kuondoka China ukitulia na thamani ya sarafu ya China RMB ikiongezeka.

    Mchumi wa kitengo cha China cha benki hiyo Bw. Li Weiqiao amesema China imedumisha ustahimilivu kwenye uchumi na kuimarisha nguvu ya kuendeleza mageuzi, ambapo serikali ya China imetoa sera na hatua mbalimbali za udhibiti kwa lengo la kutimiza uwiano wa uchumi na kuepusha hatari za kifedha, kwenye msingi wa kutoathiri kidhahiri ukuaji wa uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako