• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Marekani kushughulikia kwa busara uhusiano kati ya pande mbili

    (GMT+08:00) 2017-12-19 18:47:03

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, China inaitaka Marekani kuacha kupotosha kwa makusudi mkakati wa China, na kushughulikia kwa busara uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Serikali ya Marekani imetoa ripoti ya mkakati wa usalama wa taifa ikikosoa mambo ya ndani na sera za kidiplomasia za China na kusema China ni mshindani wa Marekani.

    Bibi Hua amesema, China na Marekani zikiwa ni nchi kubwa zaidi inayoendelea na nchi kubwa zaidi iliyoendelea duniani, zina wajibu wa pamoja wa kulinda amani na utulivu wa dunia na kuhimiza ustawi na maendeleo ya dunia na kusimamia maslahi ya pamoja ya nchi hizo. Amesema ushirikiano ni chaguo pekee sahihi kwa nchi hizo mbili, na kunufaishana ni njia pekee inayoweza kujenga mustakbali bora wa siku za baadaye.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako