• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Falme za kiarabu walaani shambulizi la kombora la Houthi dhidi ya Riyadh

    (GMT+08:00) 2017-12-20 08:49:18

    Umoja wa Falme za kiarabu UAE umelaani vikali shambulizi la kombora lililofanywa na kundi la Houthi dhidi ya mji wa Riyadh, Saudi Arabia. Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa ya nchi hiyo imesema shambulizi hilo linatishia amani na usalama kwenye kanda hiyo, na kusisitiza kuwa Umoja wa Falme za kiarabu unaiunga mkono kithabiti Saudi Arabia dhidi ya mtu yeyote anayejaribu kutishia usalama au kuharibu amani na utulivu wa nchi hiyo. Hii ni mara ya tatu kwa Riyadh kushambuliwa baada ya roketi mbili kurushwa kutoka Yemen mwezi Mei na Novemba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako