• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la umoja wa mataifa kufanya mkutano wa dharura kuhusu Jerusalem baada ya azimio kupigiwa kura ya turufu

    (GMT+08:00) 2017-12-20 08:55:12

    Umoja wa mataifa utaitisha mkutano maalum wa baraza la umoja huo kuhusu Jerusalem, baada ya Marekani kuipigia kura ya turufu rasimu ya azimio lililopendekezwa na Misri, lenye lengo la kuitaka Marekani ibadilishe uamuzi wake wa kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.

    Mjumbe wa Palestina Bw Riyad Mansour ameeleza matumaini yake kuwa baraza la Umoja wa mataifa litapitisha azimio la kumtaka Rais Donald Trump wa Marekani aondoe uamuzi wa Marekani.

    Si kawaida kwa umoja wa mataifa kuitisha mkutano maalum. Hatua hii imefikiwa baada mwenyekiti wa baraza la umoja wa mataifa Bw. Mirislav Lajack, kukutana na maofisa wa nchi za kiarabu, muda mfupi baada ya Marekani kuipiga kura ya turufu rasimu iliyopendekezwa na Misri, huku wajumbe wengine wote wakiipigia kura ya ndio.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako