• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la usalama la umoja wa mataifa laidhinisha tena misaada ya kuvuka mpaka

    (GMT+08:00) 2017-12-20 08:55:33

    Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limepitisha azimio la kuruhusu upya utoaji wa misaada ya kibinadamu ya kuvuka mpaka nchini Syria kwa kipindi cha miezi 12 hadi Januari 10, mwaka kesho.

    Azimio hilo linaitaka serikali ya Syria kujibu haraka maombi yote ya utoaji misaada ya kuvuka mpaka, yanayotolewa na umoja wa mataifa na wadau watekelezaji. Azimio hilo pia linamtaka katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bw. Antonio Guterres kufanya tathmini ndani ya miezi sita tangu kupitishwa kwa azimio, kutoa mapitio ya utekelezaji wake, ikiwa ni pamoja na mapendekezo ya namna ya kuimarisha utaratibu wa usimamizi wa umoja wa mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako