• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa mmoja auawa kwenye shambulizi la kigaidi dhidi ya uwanja wa ndege wa Sinai, Misri

    (GMT+08:00) 2017-12-20 09:15:05

    Ofisa mmoja ameuawa na wengine wawili wamejeruhiwa kwenye shambulizi la kigaidi dhidi ya uwanja wa ndege wa mji wa Arish, katika mkoa wa Sinai Kaskazini unaopakana na Israel na ukanda wa Gaza wa Palestina.

    Msemaji wa jeshi la Misri Tamer al-Refaay ametoa taarifa akisema, shambulizi hilo lilitokea jana wakati mawaziri wa ulinzi na mambo ya ndani walipofanya ziara mjini Arish na kukagua hali ya usalama mjini humo.

    Mashambulizi ya kigaidi nchini Misri yamesababisha vifo vya mamia ya polisi na askari, tangu jeshi la Misri kumwondoa madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo Bw. Mohamed Morsi mwezi Julai mwaka 2013.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako