• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Conte ashtushwa na suala la Djik kwenda kujiunga na Manchester City

  (GMT+08:00) 2017-12-20 09:45:29

  Tetesi zilizozagaa kwa sasa ni kwamba baada ya wiki kadhaa mlinzi wa klabu ya Southampton Virgil Van Djik atakwenda Etihad kumwaga wino kuitumikia City, jambo hilo limemshtua sana kocha wa Chelsea Antonio Conte.

  Conte ametishwa na suala la Djik kwenda kujiunga na Manchester City na anaamini kama jambo hilo litatokea basi itakuwa ngumu kwa wapinzani wa Man City kushindana nao na itawaumiza wengi.

  Antonio Conte ameviambia vilabu vingine kwamba kama City wakichukua kila mchezaji bora itakuwa ngumu kuwazuia, Conte amesisitiza kwamba vilabu vingine vijaribu kuwapa City upinzani kwa Djik.

  Djik alikuwa benchi katika mchezo kati ya Chelsea na Southampton mwishoni mwa wiki iliyopita na tayari kocha wa Southampton Maurcio Pellegrino amethibitisha kwa Djik anaweza kuondoka January.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako