• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Changamoto kuu za kijamii nchini China zinabadilika na kutoa fursa mpya kwa makampuni

    (GMT+08:00) 2017-12-20 16:37:41

    Ripoti ya mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China inaeleza kuwa ujamaa wenye umaalum wa kichina umeingia katika zama mpya, na changamoto kuu za kijamii nchini China zimekuwa pengo kati ya mahitaji ya wananchi ya maisha bora na maendeleo yanayokosa uwiano na ujumuishi. Wachambuzi wanaona kuwa mabadiliko ya changamoto kuu za kijamii nchini China yatatoa fursa mpya za kibiashara kwa makampuni.

    Katika miaka ya hivi karibuni, habari kuhusu "wachina kwenda nje ya nchi kununua kwa wingi maziwa ya unga na rice cooker" zinasikika mara kwa mara. Lakini hali halisi ni kuwa China imekuwa na uwezo wa kuzalisha bidhaa hizo, na hata uzalishaji huo umekuwa mwingi kupita kiasi. Waziri wa viwanda na teknolojia wa China Miao Wei anasema,

    "Hali hii imeonesha tatizo letu katika utoaji bidhaa, japokuwa uzalishaji wetu ni mwingi katika sekta nyingi, lakini mahitaji ya bidhaa za hali ya juu bado hayajakidhiwa."

    Naibu mwanauchumi mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Mawasiliano ya Uchumi cha China Xu Hongcai anaona kuwa mahitaji mbalimbali ya wananchi na maisha bora hayawezi kukidhiwa kutokana na ukosefu wa ubora na ufanisi wa bidhaa zinazotolewa.

    "Hivi sasa mahitaji ya wananchi katika manunuzi yamekuwa ya aina mbalimbali, jambo ambalo haliwezi kutimizwa, lakini maeneo hayo yataweza kupewa kipaumbele kwa uwekezaji wa makampuni yetu. Tunapaswa kupata uwezo mpya wa kuzalisha na kukidhi mabadiliko ya mahitaji ya wananchi. Makampuni yanapaswa kuweka kipaumbele kwenye ubora na ufanisi wa bidhaa, kuinua ubora wa bidhaa na huduma, na kushika vizuri fursa mpya za kibiashara, ili kukuza biashara zao."

    Msimamizi wa kampuni moja iliyoko mjini Jiaxing, mashariki mwa China Bw. Shou anasema makampuni yanatakiwa kutilia maanani ubora ili kutatua changamoto katika utoaji na mahitaji ya bidhaa.

    "Zamani bidhaa ikizalishwa, bila shaka kulikuwa na mteja atakayeinunua. Lakini sasa hali imebadilika, kama ubora haufikii vigezo, wateja watanunua kutoka nje ya nchi, bila kujali wanatumia pesa kiasi gani. Lakini hii pia inaonesha kuwa kama makampuni ya China yakiangalia zaidi ubora na kuongeza matumizi katika utafiti, badala ya kuangalia uzalishaji tu, tutaweza kupata wateja hao. Naweza kusema soko lipo, cha muhimu ni ubora."

    Mtaalamu wa masuala ya China katika Mfuko wa Ulaya na Sera za Kidiplomasia wa Ugiriki Gorgos Tzogopoulos amesema mabadiliko ya changamoto kuu za kijamii nchini China yametoa fursa kwa makampuni kujiboresha, na hatimaye kuwanufaisha wateja wa dunia nzima.

    "Mabadiliko hayo ni changamoto kwa makampuni ya ndani ya China, lakini pia yanaweza kuyasaidia kuinua ubora wa bidhaa zao, hii ina maana muhimu kwa wateja wa China, na pia itawavutia wateja wengi wa nchi za nje."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako