• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tibet yaahidi kuondoa watu zaidi ya laki moja kwenye umasikini mwaka ujao

    (GMT+08:00) 2017-12-20 18:09:59

    Mkoa unaojiendesha wa Tibet ulioko kusini magharibi mwa China umeahidi kuondoa watu zaidi ya laki moja kwenye umasikini mwaka ujao.

    Mamlaka ya mkoa huo imepanga kuondoa vijiji elfu mbili na wilaya 25 kutoka kwenye orodha ya nchi ya maeneo masikini. Kuanzia mwaka jana mpaka mwaka 2020, Tibet imepanga kuwekeza dola za kimarekani bilioni 30 kuondoa umasikini, huku asilimia 90 ya uwekezaji ikielekezwa kwenye miundombinu na miradi ya kuondoa umasikini katika maeneo masikini zaidi. Pia mkoa huo utaongeza kasi ya uhamishaji ili kusaidia watu wengi zaidi kuishi maisha bora.

    China inalenga kujenga jamii yenye ustawi wa kati katika nyanja zote itakapofika mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako