• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lataka juhudi zaidi ziongezwe katika kuleta utulivu nchini Lebanon

    (GMT+08:00) 2017-12-20 18:11:24

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito wa juhudi za kikanda zifanyike ili kuleta utulivu nchini Lebanon, na kuvitaka vyama vya siasa nchini humo kutojihusisha na migogoro ya nje.

    Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Baraza hilo limempongeza waziri mkuu wa Lebanon Saad Hariri kwa kurejea nchini humo na uamuzi wake wa kuendelea na wadhifa wake, huku likithibitisha tena kuunga mkono utulivu, usalama, ukamilifu wa ardhi, mamlaka, na uhuru wa kisiasa wa Lebanon.

    Taarifa hiyo imesema, Baraza hilo limezitaka nchi na mashirika katika kanda hiyo kufanya kazi kwa ajili ya utulivu na usalama wa Lebanon, na kuheshimu mamlaka yake na ukamilifu wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako