• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China hailengi kutafuta uongozi kwa kupitia kuhimiza pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja"

    (GMT+08:00) 2017-12-20 18:42:19

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo hapa Beijing amesema, China inashikilia kanuni za kujadiliana, kujenga na kunufaishana kwa pamoja kwenye kusukuma mbele pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", na haitafuti kuunda kanuni ya nchi moja kuongoza.

    Bibi Hua amesema, pendekezo hilo halitaunda kundi la nchi, wala halilengi nchi yoyote, na kwamba ni pendekezo lenye uwazi na ujumuishi. Ameongeza kuwa China inakaribisha pande mbalimbali kushiriki kwenye pendekezo hilo, huku ikitaka pande husika kushughulikia pendekezo hilo kwa busara.

    Pia amesema, pendekezo hilo linalenga kuhimiza ujenzi wa miundombinu na mawasiliano katika nchi zinazoshiriki kwenye pendekezo hilo, na kuunganisha sera na mkakati wa maendeleo wa nchi mbalimbali, ili kutimiza maendeleo ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako